Kiswahili

NBS2GO katika Kiswahili



Jinsi Ya Kuanzisha Kikundi Cha Kusoma Bibilia

Tuna amini kwamba Mwenyezi Mungu angependa kukutumia wewe jinsi ulivyo na mahali unapo ishi, unapofanya kazi na unako jumuika na watu, ili kutimiza mambo makuu ya milele. Ili kuanza, tizama orodha hii ya mambo matatu rahisi:

1. OMBA

… huanza kwa maombi na uhusiano

MAOMBI
● Muombee mwenzako atakaye kusaidia kuanzisha kikundi cha Somo hili La Bibilia.
● Ombeni pamoja mara kwa mara. Muulize Mungu awape mpango wake na mwelekeo.
● Waombeeni watu kwa kutaja majina yao. Ombeni Mumgu awape fursa za kupatana nao, kuwajali na kuwatumikia
● Waombeeni wapate hamu ya kusoma Bibilia.

UHUSIANO
● Kutana na majirani wako wanao ishi, wanao fanya kazi na wanao jumuika karibu na wewe. Kuwa rafiki mwema kwao na uwape motisha.
● Anzisha mazungumzo – waulize maswali na uwape sikio lako (skiza kwa umakini).
● Jumuikeni pamoja kwa kikombe cha chai, kahawa au chakula.
● Tafuta fursa ya kuonyesha upendo na kuwatumikia.

2. UNGANA

… watafute walio na hamu ya kujiunga

PANGA MKUTANO
● Panga siku, saa na kikao cha mkutano.
● Tengeza orodha ya wale wangependa kuhudhuria mkutano.
● Omba, kisha uwaalike.
● Fanya mpango wa kuandaa kiburudisho kama ingewezekana.
● Tengeza orodha ya mpangilio wa mkutano (mambo ya kufanya kwenye mkutano).

MUONGOZO WA MKUTANO
● Kama inahitajika, andaa kiburudisho kama chai, kahawa au matunda.
● Wakaribishe walio hudhuria na ujitambulishe ili muweze kujuana. Jumuika pamoja kwa kuulizana maswali, kuimba nyimbo, au michezo ya ucheshi ili kujuana zaidi.
● Mnapo malizia mkutano, wapongeze wageni kwa kuhudhuria. Unaweza ukatumia
maneno yafuatayo kwa hotuba yako: “Umekua wakati mzuri sana kwetu sisi kujumuika pamoja. Ni matumaini yangu na lengo langu kuona sisi kama jamii tuki ishi kwa umoja na upendo, na kusoma Bibilia pamoja ili kuelewa jinsi inavyosema, na kupata ufunuo wa kuelewavile la Mungu linatushusu sisi binafsi. Je, wewe ungependa kushuhudia mambo haya?”

3. ONGOZA

… sasa anza

● Pakua na uchapishe Mwongozo wa Kusoma na umpe kila mtu nakala yake.
● Chagua somo moja la Bibilia kati ya sehemu nne za Maandiko Yaliyopendekezwa katika Mwongozo huo wa Kusoma.
● Wahusika watahitaji kijitabu kidogo cha kunakili kurasa walilosoma kibinafsi kila wiki.
● Mkutano wa kwanza wa somo la Bibilia:
○ Someni kwa pamoja somo la wiki ya kwanza kisha mjadiliane maswali ya siku tano za wiki kama kikundi. Hii itaonyesha jinsi ilivyo rahisikutumia somo la kibinafsi na itawezesha kiongozi kuongoza mjadala wa Bibilia kulingana na majibu ya washirika.
○ Wapatie washirika somo la wiki ya pili na uwahimize kukamilisha maswali ya siku tano za wiki, kabla ya wiki ifuatayo.

Mafunzo ya Biblia kwa Kiswahili

MWANGA (Swahili – Light)

MWANGA Maisha kwa kasa wa bahari iko katika bahari. Kifo ni lazima wanapotengwa na mazingara yao ya asili na mwangaza wowote wa bandia. Yesu alisema,” Mimi ni Nuru ya ulimwengu….na nuru inayoongoza katika uzima” John 8;12.Chambua masomo manne juu ya maisha, mahusiano, miujiza, na ujumbe wa Yesu.

Study Guide: View | Download
Leader Guide: View | Download
Duration: 8 week

MOYO (Swahili – Heart)

MOYO: Neno la Mungu linabadilisha mioyo! Masomo mawili ya kwanza ya “MOYO” inalenga moyo wa Mungu kwa ajili yako najinsi moyo wako unaweza kuwa nyumba ya Kristo. Masomo mawili ya mwisho inakuongoza kuchimbua vifungu ambavyo vitahimiza na kuimarisha moyo wako. Masomo haya ya Biblia ya Siku 5 hutoka kwa vifungo aina mbalimbali vya Agano la Kale na vya Agano Jipya.

Study Guide: View | Download
Leader Guide: View | Download
Duration: 8 week